×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jaji Marete Njagi anayewania wadhifa wa Jaji Mkuu ajitetea kwamba hana matatizo ya kiakili

Jaji Marete Njagi anayewania wadhifa wa Jaji Mkuu ajitetea kwamba hana matatizo ya kiakili

Jaji Marete Njagi anayehojiwa katika wadhfa wa Jaji Mkuu amelazimika kufafanua kwamba hana matatizo ya akili, jinsi cheti chake cha kuthibitisha kwamba ni mtu mwenye ulemavu kinavyosema.

Akijibu maswali ya  Mohammed Warsame, Jaji Marete amesema kulikuwa na tatizo wakati aliposajiliwa kukichukua cheti hicho, na kwamba tatizo alilo nalo ni la macho pia anaugua kisukari na wala si la akili.

Jaji Njagi amesema matatizo ya kiafya aliyonayo hayajamzuia kutekeleza majukumu yake hadi sasa na hayawezi kumzuia kutekeleza wajibu wake iwapo ataidhinishwa kuwa Jaji Mkuu.

Suala jingine ambalo limejitokeza ni  mvutano ambao umekuwapo baina ya Jaji Marete na Idara ya Mahakama kuhusu marupurupu ya msaidizi wake kutokana na hali yake ya afya. Amesema marupurupu anayopewa ya shilingi elfu ishirini ya watu wenye ulemavu anayopewa hayatoshi.

Jaji Marete ni wanne kuhojiwa baada ya Jaji Martha Koome, Patricia Mbote na Chitembwe Said Juma.

Share this: