×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mfanyakazi wa KBC Betty Barasa azikwa

Mfanyakazi wa KBC Betty Barasa azikwa

Mfanyakazi wa Idhaa ya Kitaifa, KBC aliyeuliwa nyumbani kwake, Betty Barasa amezikwa leo nyumbani kwake katika eneo la Oloolua, Ngong.

Ibada ya mazishi imefanyika katika Hifadhi ya Maiti ya Montezuma kabla ya mwili kuzikwa katika mazishi ya binafsi iliyofanywa kulingana na mwongozo wa kuzuia maambukizi ya korona.

Shemejiye Edwin Namachanja ameiongoza familia kumwomboleza Betty huku akimtaja kuwa aliyependwa na watu wengi.

Barasa ambaye alikuwa mhariri wa video ameometajwa na jamaa, familia na marafiki kuwa mtu aliyewajali wenzake kila wakati.

Marehemu aliuliwa Aprili saba nyumbani kwake saa mbili usiku na majambazi waliomvizia kabla ya kumpiga risasi chumbani. Viongozi waliohudhuria mazishi yake wametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa haraka na kuwakamata waliomuua.

Haya yanajiri huku polisi wakisema uchunguzi unaendelea kuwasaka waliomuua. Mumewe na kijakazi waliokuwa nyumbani wakati wa kisa hicho pia wamerekodi taarifa. Aidha simu ambayo majambazi hao waliangusha walipokuwa wakitoroka inachunguzwa.

Share this: