×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Marufuku yakuwa nje kutekelezwa hadi Mei 29

Marufuku yakuwa nje kutekelezwa hadi Mei 29

Utekelezaji wa amri ya kutokuwa nje nyakati za usiku iliyowekwa na serikali ili kukabili maambukizi ya virusi vya korona utakamilika tarehe 29 mwezi wa Mei.

Kupitia tangazo katika Gazeti Rasmi la Serikali, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i amesema muda huo unajumuisha amri zote kwenye kaunti zilizotajwa kuathiriwa zaidi na korona, ambapo hutekelezwa kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri vilevile kwenye maeneo mengine nchini ambako huanza kutekelezwa kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri, yaani mwisho wa amri hizo zote ukakuwa Mei 29.

Kaunti ambazo ziliwekewa amri ya kutokuwa nje kuanzia saa mbili usiku ni Nairobi, Kiambu, Machakos, Nakuru vilevile Kajiado. Ikumbukwe Rais Uhuru Kenyatta alipiga marufuku shughuli za ibada kwenye kaunti hizi kwa muda usiojulikana.

Kupitia tangazo hilo Matiang'i amesema amri hiyo iliwekwa kwa muda wa siku sitini.

Awali kwenye tangazo katika gazeti lilo hilo la serikali, amri ya kutokuwa nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri ilipaswa kuendelea kutekelezwa kwa muda wa siku thelathini zaidi kote nchini baada ya muda wa siku 60 kukamilika.

Matiang'i aidha amewajumuisha mawakili vilevile wale wanaotoa huduma za kuwaokoa watoto wanaokumbwa na dhuluma za kijinsia katika orodha ya watu wanaotoa huduma muhimu na ambao wanaruhusiwa kuendeleza shughuli zao wakati wa kutekelezwa kwa masharti ya kukabili korona.

Share this: