×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mahakama ya Runyenjes yafungwa kwa wiki moja kufutia maambukizi

Mahakama ya Runyenjes yafungwa kwa wiki moja kufutia maambukizi

Mahakama ya Runyenjes kwenye Kaunti ya Embu imefungwa kwa kipindi cha wiki moja baada ya wafanyakazi kumi na wanane kuambukizwa virusi vya korona.

Kupitia taarifa, Kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu amesema kwamba shughuli ya kupuliza dawa kwenye majengo ya mahakama hiyo itafanyika wakati wa kipindi hicho. Mwilu aidha amesema kwamba waathiriwa wameagizwa kujitenga kuendena na mwongozo wa kuzuia maambukizi.

Maafisa wa afya waliitembelea mahakama hiyo wiki iliyopita na baada ya kuwafanyia vipimo wafanyakazi waliagiza mahakama kufungwa.

Mwilu vilevile amesema kuwa wafanyakazi wengine watapimwa kubaini iwapo wameambukizwa virusi hivyo au la.
Kwa sasa kesi za dharura zilizokuwa zikishughulikiwa na Mahakama ya Runyenjes zimeelekezwa katika Mahakama za Kerugoya na Embu.

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya Mahakama ya Karatina kufungwa kwa siku kumi baada ya afisa mmoja wa mahakama kuthibitishwa kuambukizwa huku wengine 16 wakitengwa.

Share this: