×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ukur Yattani kuhojiwa kuhusu mchakato wa mkopo wa shilingi bilioni 225

Ukur Yattani kuhojiwa kuhusu mchakato wa mkopo wa shilingi bilioni 225

Waziri wa Fedha Ukur Yattani asubuhi hii anatarajwa kufika mbele ya kamati mbili za bunge kufafanua mchakato wa serikali kukopa kima cha shilingi bilioni 225 kutoka kwa Shirika l a Fedha Duniani, IMF.

Yatani anatarajiwa kuhojiwa na wanakamati za Bajeti na Fedha kuhusu deni hilo ambalo liliibua mjadala mkubwa miongoni mwa Wakenya ambao wanahisi utawala wa Jubilee umeendeleza hulka ya kukopa kutoka mataifa na mashirika ya nje na hivyo kuwabebesha walipa kodi mzigo mzito.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Kanini Kega amesema kwamba miongoni mwa masuali ambayo watamuuliza Yatani ni kuhusu mpango wa serikali kuyalipa madeni yake pamoja na mikataba kati ya Kenya na mashirika hayo kuhusu mikopo hiyo.

Hapa Radio Maisha ni matumaini yetu kwamba Waziri Yatani ataweka wazi madhumuni ya utawala wa Rais Uhuru Kenyatta kuendeleza hulka ya kukopa na vilevile kuweka wazi mikataba kati ya taifa hili linalojivunia miaka 56 ya kujitawala na mashirika hayo.

Aidha, Wakenya tayari wameelezea kutoridhishwa kwao na jinsi mikopo ya awali ilivyotumika, ishara tosha kwamba imani yao katika serikali hii inaendelea kudidimia hususan katika suala zima la usimamizi wa fedha za umma.

Je, uwapi mkataba kati ya Benki Exim ya Uchina na serikali ya Kenya kuhusu kujengwa kwa Reli ya Kisasa, SGR 

Share this: