×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

26 waaga dunia na 991 wakiambukizwa Korona Kenya chanjo ikiendelea

26 waaga dunia na 991 wakiambukizwa Korona Kenya chanjo ikiendelea

Watu 991 wamethibitishwa Jumanne kuambukikizwa virusi vya Korona katika saa 24 zilizopita, hivyo kufanya idadi jumla ya walioambukizwa kuwa 147, 147.

Takwimu hizo zimetokana na vipimo vya sampuli 6, 417 ambapo viwango vya maambukizi ni asilimia 15. 6 kulinganishwa na asilimia 11. 8 ya siku iliyotangulia.

Miongoni mwa walioambukizwa, 956 ni Wakenya, 35  wakiwa raia wa kigeni.

Aidha, aliye mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi 7  na mkongwe wa miaka 99.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza ambapo 296 wameambukizwa, Kiambu 67, Kericho 58 na Nakuru 44.

Wakati uo huo, watu 370 wamepona Ugonjwa wa COVID-19 na kufanya idadi jumla ya waliopona kuwa 99,580.

Miongoni mwa waliopona, 214 walihudumiwa nyumbani na 156 ni waliolazwa katika hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, watu wengine 26 wameripotiwa kuaga dunia katika saa 24 zilizopita kutokana na makali ya COVID-19.

Kufikia sasa jumla ya watu waliokufa kutokana na korona nchini Kenya ni 2, 394.

Kuhusu chanjo, kufikia Jumatatu tarehe 12 Aprili, jumla ya watu 526, 026 walikuwa wamepewa chanjo ya Astrazeneca.

Share this: