×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wahariri waanzisha mpango wa kuwaelimisha wanahabari Afrika

Wahariri waanzisha mpango wa kuwaelimisha wanahabari Afrika

Baraza la Wahariri limeanzisha mpango wa utoaji mafunzo kwa wanahabari katika Bara la Afrika.

Mafunzo hayo yatajumuisha jinsi watakavyojikinga dhidi ya virusi vya Korona hasa wakati huu ambapo mataifa mengi yanashuhudia wimbi la tatu la maambukizi.

Katika taarifa, Rais wa Baraza hilo Churchill Otieno amesema mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha wanahabari wanapata taarifa muhimu na sahihi kuhusu Ugonjwa wa Covid-19.

Otieno amedokeza kwamba mafunzo hayo yatatolewa kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO.

Mafunzo hayo yatatolewa katika tarehe 14, 15, 16 hadi 19 mwezi Aprili kuanzia saa mbili saa za Afrika Mashariki.

Mafunzo yenyewe yatatolewa kwa njia ya Zoom na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wameshauriwa kuhudhuria.

Share this: