×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×
Moi na Muhoho wamtembelea Raila

Katika hatua inayoonekana kuwa mwendelezo wa mijadala ya miungano ya kisiasa, Mwenyekiti wa chama cha KANU, Gideon Moi amemtembelea Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Moi aliandamana na kaka wa Rais Uhuru Kenyatta, Muhoho Kenyatta.

Huu utakuwa mkutano wa hivi punde unaowahusu vigogo vya kisiasa. Wiki iliyopita, Naibu Kiongozi wa chama cha ODM, Wycliffe Oparanya alikutana na Naibu wa Rais William Ruto na Dr. Mukhisa Kitui kabla ya ya kukutana na Kinara wa ODM, Raila Odinga siku iliyofuata.

Mkutano huo pia ulimjuisha Gavana wa Mombasa Hassan Joho na Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa miongoni mwa wengine.

Awali, wachambuzi wa siasa walikuwa wamekata kauli kwamba Raila ametengwa na muungano wa One Kenya Alliance unaomjuisha Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Gideon Moi na Moses Wetangula.

Aidha mara kwa mara, Mudavadi na Kalonzo wamekuwa wakimtaja Raila kuwa asiyeaminika hasa kutokana na mwafaka wao katika NASA. Hata hivyo, huenda mtazamo huo ukabadilika kufuatia mkutano wa leo baina ya Raila na Gideon Moi.

Share this: