×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mahakama ya Kiambu yamtoza Kuria faini ya shilingi 75, 000

Mahakama ya Kiambu yamtoza Kuria faini ya shilingi 75, 000

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria ametozwa faini ya shilingi elfu sabini na tano na Mahakama ya Kiambu kwa kosa la kukiuka masharti ya kudhibiti korona.

Kuria amepewa adhabu hiyo baada ya kufunguliwa kesi ya kukiuka agizo la kutokuwa nje kuanzia saa mbili hadi saa kumi usiku ambapo Irungu Kanga'ata amekuwa wakili wake.

Kuria alikamatwa usiku wa kuamkia Jumanne akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kaunti ya Kiambu ambapo inadaiwa kwamba walikuwa wakinywa pombe katika eneo la Karuri Kiambaa.

Haya yanajiri huku madai yakiibuka kwamba kunaswa kwake kumechochewa kisiasa hasa kuhusu mrengo wake katika uchaguzi mdogo wa eneo Bunge la Juja.

Kuria amenaswa huku Njoroge Mburu, mgombea wa ubunge wa Juja kwa tiketi ya Chama cha Peoples Party of Kenya kinachoongozwa na Kuria vilevile kuhofiwa kutoweka katika hali ya kutatanisha.

Mburu anadaiwa kutoweka siku chache tu baada ya kuwasilisha ombi kwa Tume ya Uchaguzi IEBC akitaka tarehe ya uchaguzi uliofaa kufanyika tarehe 18 mwezi ujao kuahirishwa.

Share this: