×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Abdulkadir ameapishwa kuwa Seneta wa Garissa kumrithi babaye

Abdulkadir ameapishwa kuwa Seneta wa Garissa kumrithi babaye

Mohammed Abdulkadir Haji ameapishwa rasmi kuwa Seneta wa Garissa.

Haji ameapishwa asubuhi hii wakati wa vikao maalumu vya Seneti.

Alitangazwa kuwa Seneta wa Kaunti hiyo pasi na kufanyika kwa uchaguzi mdogo baada ya kukosa mpinzani baa da ya kuteuliwa na chama cha Jubilee kujaza nafasi ya babaye marehemu Yusuf Haji ambaye alifariki dunia Februari mwaka huu.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kwanza, Seneta Abdikadir ameahidi kuwahudumia wakazi wa Garissa na kukamilisha shughuli alizoanzisha babaye.

Meseneta wakiongozwa na Kipchumba Murkomen na Enock Wambua wamempongeza Haji kwa kuteuliwa bila kupingwa na kumtaka kuendeleza kazi aliyoanzishwa baba yake.

Abdikadir amesifiwa kwa juhudi za kuwaokoa Wakenya wakati wa Shambulio la Westgate mwaka wa 2013.

Baadhi ya viongozi wa Garissa walifika bungeni kuhudhuria kuapishwa kwake

Share this: