×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Korona kusalia katika mataifa mengi duniani, WHO yasema

Korona kusalia katika mataifa mengi duniani, WHO yasema

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema huenda Janga la Korona likasalia katika mataifa mengi iwapo raia hawatafuata masharti ya shirika hilo ya kukabili maambukuzi ya virusi hivyo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema baadhi ya mataifa tayari yamerejelea shughuli za kawaida licha ya kwamba Janga la Covid-19 lingalipo.

Hata hivyo, Tedros amedokeza kuwa  zipo sababu za kujipa moyo kwamba hali inaweza kudhibitiwa ikizingatiwa kupungua maradufu kwa idadi ya vifo vya wagonjwa wa Covid-19 hususan miezi miwili ya kwanza mwaka huu.

Wito huu unajiri wakati Shirika la Biashara Duniani, WTO kupitia Mkurugenzi Mkuu Ngozi Okonjo akiwataka viongozi wa mataifa ya bara Afrika kushirikiana kuongeza idadi ya uzalishaji wa chanjo dhidi ya Korona.

Share this: