×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Je, unamfahamu Prof. Kameri anayelenga kuwa Jaji Mkuu Kenya

Je, unamfahamu Prof. Kameri anayelenga kuwa Jaji Mkuu Kenya

Mahojiano ya kujaza wadhfa wa Jaji Mkuu mbele ya Tume ya Huduma za Mahakama JSC yameendelea kwa siku ya pili huku ikiwa zamu ya Mhadhiri na Msomi wa Sheria Prof . Patricia Kameri Mbote.

Prof. Mbote amekuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwa zaidi ya miaka 30.

Alisomea sheria katika chuo hicho kabla ya kuelekea katika Chuo Kikuu cha Warwick nchini Uingereza, Chuo Kikuu cha Zimbabwe kabla ya kupata shahada ya uzamifu kutoka Chuo Kikuu cha Stanford Marekani.

Katika sheria amejikita zaidi katika masuala ya mazingira na haki za binadamau, ambapo mbali na kuwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi amewahi kufunza katika Chuo Kikuu cha Kansasa nchini Marekani.

Amekuwa mshauri wa mashirika kadhaa ya kiamataifa likiwamo Shirika la World Bank, UNDP, Shirika la Maendeleo la Norway NORAD, na serikali ya Kenya, Pia ni Mkurugenzi Mwanzilishi wa Shirika la Mazingira la International Environmental Law Research Centre.

Ametafiti na kuchapisha tafiti kuhusu masuala mbalimbali ya sheria na kutuzwa na Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani na Chuo Kikuu cha Oslo nchini Norway.

Pia kitaifa ana hadhi ya EBS - Elder of the Burning Spear kupitia tuzo inayotolewa na Rais Uhuru Kenyatta kila mwaka. Prof Kameri Mbote ni mwanamke wa pekee katika Chuo Kikuu cha Nairobi kupata shahada ya juu ya uzamifu yaani Higher Doctorate Degree baada ya kuandika nakala ya utafiti.

Share this: