×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Chitembwe adondokwa na machozi wakati wa mchujo wa atakayekuwa Jaji Mkuu

Chitembwe adondokwa na machozi wakati wa mchujo wa atakayekuwa Jaji Mkuu

Jaji wa Mahakama Kuu, Said Juma Chitembwe anayewania wadhifa wa Jaji Mkuu amekabiliwa na wakati mgumu kuwaeleza makamishna wa Tume ya JSC jinsi alivyoaafikia uamuzi wa kumwachilia huru mwanamume aliyefungwa miaka 20 kufuatia kosa la ubakaji wa msichana wa miaka 13, alipokuwa akihudumu katika Mahakama ya Malindi.

Akihojiwa wakati wa mchujo huo ambao umeanza leo hii, Jaji Chitembwe amesisitiza kwamba japo msichana huyo alikuwa chini ya umri wa miaka 18, ushahidi ulionesha kwamba alifurahia tendo la ndoa na mwanamume huyo kwa kuwa alifanya hivyo zaidi ya mara moja.

Katika kikao hicho, Chitembwe aidha ametakiwa kueleza kuhusu jinsi atakavyoyatekeleza majukumu yake kama Jaji Mkuu ikizingatiwa kwamba aliwahi kuhusishwa na kesi ya ufisadi wa shilingi bilioni 1.37 kabla ya kuondolewa mashtaka. Ni wakati wa suali hilo, ambapo Chitembwe amelengwalengwa na machozi, alipokuwa akieleza jinsi alivyohangaishwa licha ya kuwa hakuwa na hatia.

Jaji Mohamed Warsame na Mwanasheria Mkuu wa serikali Paul Kihara ambao vilevile makamishna wa JSC, wamemtaka Chitembwe kufafanua jinsi atakavyoshughulikia hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kudinda kuwaidhinisha majaji arubaini na wawili waliopendekezwa na Tume ya Huduma za Mahakama.

Aidha kauli yake kuwa amekuwa akijitolea kuitumikia idara hiyo kiasi cha kuugua ugonjwa wa kisukari imemweka pabaya, baada ya Warsame kutilia shaka uwezo wake wa kuyatekeleza majukumu ya Jaji Mkuu ambaye huwa na kazi chungu nzima za kuingoza idara ya mahakama.

Kuhusu suala la ufisadi katika Idara ya Mahakama , Chitembwe amesema linaweza kukabiliwa iwapo kesi zinazowasilishwa kortini zitasikilizwa na kuamuliwa kwa wakati vilevile kutumika kwa teknolojia katika kufanya malipo mahakamani.

Chitembwe amesema kuwa Wakenya wengi wamekuwa na dhana kuwa muda huo, hutumiwa kuwahonga majaji kabla ya kutoa uamuzi.

Akijibu swali la Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Kihara kuhus jinsi anavyopanga kuondoa dhana kwamba uamuzi wa mahakama umekuwa ukichochewa na ufisadi, Jaji Chitemwa aidha amesema atajaribu kadri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa shughuli zote za malipo zinafanyika kupitia teknolojia ya kisasa ili kuepusha hali ambapo fedha hupitia mikononi mwa maafisa wa idara hiyo.

Wakati uo huo Kamishna Patrick Gichohi ambaye anaiwalikisha Tume ya Huduma za Umma PSC katika Tume ya JSC ametaka kujua jinsi Chitembwe anavyopanga kushughulikia suala la kutengewa bajati ndogo ya Idara ya Mahakama na hivyo kuathiri shughuli mbalimbali. Chitembwe amefafanua kwamba suluhu kuu ni kufanya mashauriano na Kamati ya Bunge ya Fedha kuhusu umuhimu wa kutengewa bajeti kubwa ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya idara hiyo.

Aidha amesema ataihusisha Hazina Kuu ya Kitaifa kuhusu changamoto za kifedha katika idara hiyo. Hata hivyo amekumbwa na wakati mgumu kuhusu iwapo anajua bajeti kamili ya Idara ya Mahakama.

Hata hivyo Jaji Said Chitembwe ametetea hatua yake ya kukosa kulipa kodi, jinsi ilivyobainishwa na Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA.

Kwa mujibu wa Chitembwe, Tume ya Idara ya Mahakama ilipotangaza nafasi ya Jaji Mkuu kuwa wazi, aliifahamisha KRA kuhusu stakabadhi zake ambapo alibaini kwamba baadhi ya malipo ya umeme hayakuwa yamelipwa.

Akijitetea, Chitemwe aidha amesema alilipa faini ya shilingi elfu mia moja kumi na mbili kwa KRA. Aidha amesema mkewe amekuwa akilipa kodi wa kila mali anayomiliki na kwamba haelewi ni kwa nini KRA iliiambia JSC kwamba hajakuwa akilipa kodi.

Baada ya kuhojiwa kwa wawaniaji wote, JSC itachukua muda wa siku saba kuandaa ripoti ya kila mwaniaji, kisha baadae kupendekeza majina matatu kwa Rais ambaye atamteua Jaji Mkuu na kuwasilisha jina lake bungeni.

Share this: