×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

JSC kuwahoji waliotuma maombi ya wadhfa wa Jaji Mkuu kuanzia Jumatatu

JSC kuwahoji waliotuma maombi ya wadhfa wa Jaji Mkuu kuanzia Jumatatu

Maandalizi yote yamekamilika kuelekea shughuli ya kuwahoji waliotuma maombi ya wadhifa wa Jaji Mkuu vilevile Jaji wa Mahakama ya Juu.

Akiwahutubia wanahabari mapema leo, Msajili wa Idara ya Mahakama Ann Amadi amesema kila mwaniaji atahojiwa kwa takribani saa nne. Shughuli hiyo itaanza mapema kesho saa tatu asubuhi na kuendeshwa na Makamishna sita wa Tume ya Huduma za Mahakama JSC. Amewahimiza Wakenya kufuatilia shughuli hiyo kupitia mtandao wa facebook JSC vilevile kwenye Runinga.

Baada ya shughuli hiyo ambayo itadumu kwa muda wa wiki mbili, Tume ya JSC itachukua muda mwingine wa siku saba kuiandika ripoti kuhusu mchujo huo kabla ya kupendekeza majina ya wawaniaji walioibuka bora kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye baada ya kufanya uteuzi atayawasilisha majina bungeni.

Kuhusu ombi la wakili Philip Murugor ambaye ni miongoni mwa wanaowania wadhifa wa Jaji Mkuu la kutaka kumzuia Kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kuwa miongoni mwa makamishna watakaoendesha shughuli hiyo, Amadi amesisitiza kwamba makamishna wote sita watashiriki shughuli hiyo.

Murugor aliwasilisha ombi hilo akidai kwamba huenda kukawa na upendeleo ama mwingilio wa kimajukumu iwapo Mwilu atahusika kwa kuwa ni mlalamishi katika kesi ambayo wakili wake Nelson Havi anakabiliana na Fred Ngatia ambaye ni miongoni mwa wanaowania wadhifa huo.

Walioidhinishwa kuchujwa ni majaji  Said Chitembwe, Martha Koome, Marete Njagi, Philip Murgor,  Nduma Nderi, Fred Ngatia, William Ouko, Prof. Wekesa Moni, Alice Yano na Prof. Patricia Mbote.  

Wa kwanza kuchujwa ni Jaji Chitembwe tarehe 12 Aprili, yaani Jumatatu wiki ijayo kuanzia saa tatu asubuhi.

JSC aidha imetangaza tarehe 26 hadi 30 Aprili kuwa ya kuwachuja wanaowania wadhifa wa jaji katika Mahakama ya Juu. Wadhifa huo uliachwa wazi kufuatia kustaafu kwa Jaji Jackton Boma Ojwang. 

Share this: