×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 490 wamepona huku 18 wakiaga duinia kufuatia korona

Watu 490 wamepona huku 18 wakiaga duinia kufuatia korona

Viwango vya maambukizi ya korona leo hii vimeshuka hadi asilimia 11.8.

Leo hii watu mia nne themanini na sita wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli elfu nne mia moja thelathini na tatu katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi Jumla ya maambukizi humu nchini imefikia watu elfu mia moja arubaini na tano mia sita sabaini.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni elfu moja mia sita sitini na wengine elfu tano mia tisa tisini na wanne wakihudumiwa nyumbani.

Wakati uo huo wagonjwa mia nne tisini wamepona baada ya kuambukizwa korona hivyo kufikisha idadai jumla kuwa elfu tisini na tisa na tisini na tano.

Mia tatu kumi na wanane miongoni mwa waliopona walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali na wengine mia moja sabini na mbili walikuwa wakihudumiwa nyumbani.

Watu wengine kumi na wanane wamethibitishwa kufariki dunia kufikisha idadai jumla sasa kuwa elfu mbili mia tatau arubaini na nane.

Wizara ay Afya imesema wawili miongoni mwa kumi na wanane hao walifariki dunia katika saa ishirini na nne zilizopiya kumi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita na sita ripoti zao zilitolewa kuchelewa kwenye hopsutali mbalimbali.

Takwimu hizo za Wizara ya Afya zinaonesha kwamba idadi ya watu wenye umri wa miaka sitini wanaofariki kutokana na korona ni ya juu zaidi ambao ni watu elfu moja mia moja na ishirini na nane, wanafuatwa na walio na miaka kati ya hamsini na hamsini na tisa kisha arubaini na arubaini na tisa, huku kiwango cha chini cha vifo kikiripotiwa miongoni mwa walio na kati ya umri wa miaka kumi na kumi na tisa.

Share this: