×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wasafiri kutoka Kenya kuelekea Irelanda watakaa karantini

Wasafiri kutoka Kenya kuelekea Irelanda watakaa karantini

Kenya ni miongoni mwa mataifa yaliyoongezwa katika orodha ambayo wasafiri wake watahitajika kukaa karantini baada ya kufika Ireland.

Kupitia mtandao wa Twitter, Ubalozi wa Ireland umesema wasafiri wote kutoka Kenya lazima wakae karantini ya lazima katika hoteli ambazo watajiandikisha kabla ya kusafiri.

Ubalozi huo umesema agizo hilo litaanza kutekelezwa tarehe 15 mwezi huu ambapo ni siku ya Alhamisi wiki hii.

Kulingana masharti hayo wasafiri wote watahitajika kukaa kwa siku kumi kabla ya kufanyiwa vipimo ili kubaini iwapo wana korona au la.

Iwapo matokeo yatabainika kwamba hawana basi wataruhusiwa kukamilisha kipindi cha karantini nyumbani ambacho ni siku kumi na nne.

Mataifa mengine yaliyo katika orodha hiyo ni Marekani, Canada, Ubelgiji na Ufaransa.

 

Share this: