×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

1030 waambukizwa korona, 21 wafariki

1030 waambukizwa korona, 21 wafariki

Watu wengine elfu moja na thelathini wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona leo hii.

Idadi hii imetokana na sampuli elfu nane, mia tatu kumi na sita zilizopimwa katika saa ishirini na nne zilizopita.

Miongoni mwa walioambukizwa, mia tisa tisini na watano ni Wakenya huku thelathini na watano wakiwa raia wa kigeni.

Aidha, mia tano thelathini na wawili ni wa kiume huku mia nne tisini na wanane wakiwa wa kike.

Mtoto wa miezi kumi na mkongwe wa miaka tisini na tisa ni miongoni mwa walioambukizwa virusi hivyo.

Viwango vya maambukizi leo hii ni asilimia 12. 4 ikilinganishwa na asilimia 14. 9 ya jana.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuna wagonjwa elfu moja, mia sita kumi na sita ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali.

Aidha, wengine elfu nne, mia mbili arubaini na watatu wanahudumiwa nyumbani.

Pia Kagwe amethibitisha kuwa wagonjwa mia mbili arubaini na saba wamelazwa katika Vyumba vya Wagonjwa Mahututi ICU, ambapo arubaini na sita miongoni mwao wanatumia vipumuzi, na wengine mia moja sabini wakiwekewa Oksijeni.

Wagonjwa thelathini na mmoja wanahitaji uangalizi wa karibu.

Wakati uo huo, Kagwe amesema watu mia nne ishirini na wawili wamepona ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha jumla ya waliopona kuwa elfu tisini na nane, mia sita na watano.

Miongoni mwa waliopona, mia tatu kumi na saba walikuwa wakihudumiwa nyumbani.

Mia moja na watano walikuwa wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini.

Hata hivyo, watu ishirini na mmoja wameaga dunia kutokana na makali ya COVID-19 na kufikisha idadi jumla ya vifo humu nchini kuwa elfu mbili, mia tatu na thelathini.

Share this: