×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Polisi Embakasi wamlilia Mutyambai awasaidie

Polisi Embakasi wamlilia Mutyambai awasaidie

Inspekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai ametumiwa barua ya malalamishi ya Maafisa wa Polisi katika Kituo cha Embakasi hapa Jijini Nairobi.

Katika barua hiyo, Mutyambai amefahamishwa kuhusu mahangaiko ya maafisa hao wakiwa kazini, ambapo wamedai kwamba Mkuu wa Kituo cha Polisi OCS Lucy Waithera amekuwa akiwadhulumu kila mara.

Aidha, maafisa wa kitengo cha Uchunguzi wa kesi za uhalifu wamesema OCS Waithera amekuwa akitatiza uchunguzi kwa kuamua washukiwa kuachiliwa huru kwa dhamana bila kufikishwa mahakamani.

Wamesema wamekuwa wakiitwa na kuhojiwa na wakuu wao bila hatua yoyote kuchukuliwa.

Inaarifiwa kwamba OCS Waithera amekuwa akiingilia kati kesi za magari yasiyokuwa na leseni, pikipiki na kesi za wizi ambapo amekuwa akiamua washukiwa kuachiliwa baada ya kutoa shilingi angalau elfu sabini bila kurekodiwa katika kitabu cha matukio.

Polisi hao wanasema Waithera amekuwa akijidai kuwa na ushawishi katika Idara ya Polisi na hata kuwatishia kuwafuta kazi iwapo watapatikana wakienda kinyume na mipango yake.

Kwa sasa maafisa hao wamemwomba Mutyambai kuingilia katika suala hilo ili kuboresha huduma za polisi kwa wananchi.

Nakala ya barua hiyo imetumwa kwa Ofisi ya Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi, Kamanda wa Nairobi na Kamanda wa Eneo la Embakasi.

Share this: