×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mataifa ya Kenya na Tanzania yalenga kuimarisha uhusiano

Mataifa ya Kenya na Tanzania yalenga kuimarisha uhusiano

Ili kuimarisha uhusiano wake Kenya na Tanzania zimebuni Kamati ya ushirikiano itakayoshughulikia uhusiano baina ya mataifa haya mawili.

Rais wa Tanzania Suluhu Samia Hassan ameagiza kubuniwa kwa kamati hiyo leo hii wakati alipofanya mkutano na Waziri wa Michezo wa Kenya Amina Mohamed aliyemwakilisha Rais Uhuru Kenyatta.

Waziri Amina ambaye ameandamana na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Dan Kazungu wamewasilisha ujumbe wa Rais Kenyatta ambaye ameahidi kushirikiana na taifa hilo jirani kwa manufaa ya raia.

Rais Samia kwa upande wake ameahidi kuendeleza urafiki wa Kenya na Tanzania ambao ulidumishwa na Hayati John Pombe Magufuli.

Samia amesema atashughulikia tofauti zote zilizopo baina ya mataifa haya mawili.

Huu ni ujumbe wa kwanza wa Rais Kenyatta tangu samia kuingia madarakani wiki chache zilizopita kufuatia kifo cha Magufuli huku akimkaribisha kufanya ziara nchini.

Share this: