×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ajuza Kaunti ya makueni ametoa wito kwa wakenya kupokea chanjo

Ajuza Kaunti ya makueni ametoa wito kwa wakenya kupokea chanjo

Ajuza mwenye umri mwa miaka 95 kwenye Kaunti ya Makueni aliyepata tuzo ya Rais ya HSC siku ya Mashujaa mwaka jana ametoa wito kwa Wakenya kuchanjwa dhidi ya virusi vya korona.

Halima Ramadhan Ndeve aliyezaliwa mwaka wa 1925, miaka saba tu baada ya dunia kukabili janga jingine la homa ya mafua Influenza mwaka wa 1918, ameishukuru serikali kwa kuhakikisha chanjo hiyo inawafikia wazee wa maeneo ya mashinani, akisema chanjo ndiyo njia mwafaka ya kukabili korona.

Nyanya huyo alituzwa kwa ushujaa wake wakati wa ukoloni kwa kuwapikia chakula wapiganaji wa MAU MAU waliopigania uhuru wa taifa.

Share this: