×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maafisa wa KDF wamewanasa makurutu wanaosambaza barua ghushi

Maafisa wa KDF wamewanasa makurutu wanaosambaza barua ghushi

Maafisa wa Jeshi la Ulinzi KDF, wamewanasa makurutu hamsini na watano na watu watatu wanaohusisha na tuhuma za kusambaza  barua ghushi za usajili wa vijana wanaojiunga na KDF.

Washukiwa wamenasa katika Chuo cha kutoa mafunzo kwa Makuruti cha Moi Barracks mjini Eldoret. Miongoni mwao ni mchungaji hapa jijini Nairobi Joseph Onyancha ambaye aliwasafirisha vijana kumi na watatu wakiwa na barua bandia ya kujiunga na KDF.

Amedai kuwa alipokea barua hizo baada ya kumpa mwanamke mmoja mfanyabiashara shilingi milioni 3.5 ili kuwasaidia vijana hao wa Kaunti ya Nyamira. 

Mwingine ni mganga Simon Isiche wa Navakholo kwenye Kaunti ya Kakamega ambaye amekuwa akijidai kuwa na ushawishi katika jeshi. Amemhadaa mkazi kuuza shamba lake na kumpa laki nne ili kumsaidia mwanawe kupata kazi hiyo.

Vijana waliokamatwa wamesema kwamba wametoa kati ya shilingi 270,000 na 400,000 ili kuwawezesha kujiunga na jeshi.

Afisa wa Kitaifa wa KDF ayesimamia shughuli za usajili mwaka huu Brigadia Peter Muteti amesema kuwa vijana hao walikuwa wamefika katika chuo hicho na barua hizo ghushi.

Muteti amesema wamekamatwa kati ya Jumatano na leo wakati shughuli za kuwapokea rasmi makurutu waliosajiliwa imekuwa ikiendelea.

Watu hao watashtakiwa uchunguzi utakapokamilika.

 

Share this: