×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gazeti lenye muonekano mpya la The Standard lazinduliwa

Gazeti lenye muonekano mpya la The Standard lazinduliwa

Asubuhi hii, Wakenya wameanza kupokea na kufurahia sura mpya ya gazeti la The Standard linalosambazwa kote nchini na mitandaoni.

Gazeti hilo lilizinduliwa jana  katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Standard kwenye barabara ya Mombasa- Nairobi. Shirika hili linalenga kuimarisha hata zaidi usambazaji wa habari za hivi punde,  za kina, zilizoandikwa kwa ufasaha na kuwasilishwa kwa njia inayozingatia usasa. 

Waziri wa Habari,Teknolojia na Mawasiliano, Joe Mucheru  alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo ambayo inaambatana na uzinduzi wa mpangilio mpya wa kufanya kazi katika mfumo wa MUUNGANIKO, yaani convergence.

Mucheru aliipongeza mikakati ilizowekwa na Standard huku akikiri kuwapo kwa changamoto kubwa katika sekta ya uanahabari na hivyo basi kuhitaji ubunifu na mawazo mapya.

Katika mpangilio huo, wanahabari wa vitengo mbalimbali kuanzia redio, runinga , gazeti na wa mtandao wanashirikiana, ambapo uzinduzi wa gazeti ni hatua moja miongoni mwa nyingine nyingi.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mtendaji wa Standard Group PLC, Orlando Lyomu ameitaja Kampuni ya Standard kuwa iliyochangia pakubwa ukuaji wa sekta ya habari kwa kuwa ya kwanza kupiga hatua katika vitengo mbalimbali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Standard, Robin Sewell aliyezungumza akiwa jijini London amesema kutakuwapo na mambo mengi mazuri kwa wateja. 

Share this: