×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Standard PLC kuzindua sura mpya ya Gazeti

Standard PLC kuzindua sura mpya ya Gazeti

Kampuni ya Habari ya Standard PLC leo inatarajiwa kuzindua sura mpya ya gazeti lake na mtandao. Katika hafla inayofanyika katika makao makuu ya Standard kwenye barabara ya Mombasa, kampuni hii inalenga kuwavutia zaidi wasomaji wake kwa habari za hivi punde, zilizoandikwa kwa ufasaha na kuwasilishwa kwa njia inayozingatia usasa.

Waziri wa Habari na Mawasiliano Joe Mucheru ni miongoni mwa wanaohudhuria hafla hii ambayo inaambatana na uzinduzi wa mpangilio mpya wa kufanya kazi.

Katika mpangilio huo, wanahabari wa vitengo mbalimbali kuanzia Radio, Televisheni, Gazeti na Mtandao watashirikiana. Ochieng Rapuro ni Mhariri Mkuu.

 

Kwa upande wake, Afisa Mkuu Mtendaji ameitaja Kampuni ya Standard kuwa iliyochangia ukuaji wa sekta ya habari kwa kuwa ya kwanza kupiga hatua katika vitengo mbalimbali.

 

Share this: