×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakili Philip Murgor amewasilisha ombi la kutaka Philomena Mwilu kuondolewa katika jopo la Tume ya Mahakama

Wakili Philip Murgor amewasilisha ombi la kutaka Philomena Mwilu kuondolewa katika jopo la Tume ya Mahakama

Wakili Philip Murgor ambaye ni miongoni mwa wanaowania wadhifa wa Jaji Mkuu amewasilisha ombi la kutaka kuondolewa kwa Kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu katika Jopo la Makamishna wa Tume ya Huduma za Mahakama watakaowachuja wawaniaji wa wadhifa huo vilevile ule wa Jaji katika Mahakama ya Juu.

Katika Ombi hilo Murgor amedai kwamba iwapo Mwilu atashiriki katika shughuli ya kuwachuja basi huenda kukawa na mwingilio wa kimajukumu kwa kuwa wakili wake ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Nelson Havi ni mlalamishi katika kesi inayomhusu Fred Ngatia ambaye ni mwaniaji wa wadhifa wa Jaji katika Mahakama ya Juu.

Ombi la Murgor linajiri wakati ambapo JSC JSC imetoa utaratibu wa kuwachuja wawaniaji kumi wa wadhifa wa Jaji Mkuu ulioachwa wazi kufuatia kustaafu wa David Maraga.

Mchujo huo utafanyika kati ya Aprili 12 na Aprili 23 huku kila mwaniaji akitengewa siku nzima ya kufanyiwa mchujo, kumaanisha kuwa kila siku, mwaniaji mmoja mmoja atachujwa.

Walioidhinishwa kuchujwa ni majaji  Said Chitembwe, Martha Koome, Marete Njagi, Philip Murgor,  Nduma Nderi, Fred Ngatia, William Ouko, Prof. Wekesa Moni, Alice Yano na Prof. Patricia Mbote.  

Wa kwanza kuchujwa ni Jaji Chitembwe tarehe 12 Aprili, yaani Jumatatu wiki ijayo kuanzia saa tatu asubuhi.

Share this: