×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Kiwanda cha Kutengeneza Silaha

Rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Kiwanda cha Kutengeneza Silaha

Rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Kiwanda cha Kutengeneza Silaha katika Eneo la Ruiru hapa Nairobi. Akizungumza katika shughuli hiyo, Kenyatta amesema janga la korona limeipa funzo serikali kuhusu uwezekano wa kucheleweshwa kwa silaha wanazoziagiza kutoka mataifa ya nje.

Amewapongeza wataalam wa humu nchini wambao wamefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kufikia sasa kimefanikiwa kutengeneza silaha elfu kumi na mbili. Kenyatta ameongeza kwamba walitumia shilingi bilioni nne pekee kinyume na bilioni kumi na tano ambazo wangetumia iwapo wangewatumia wataalam kutoka nje.

 

Aidha amesema katika muda wa miaka mitano ijayo, serikali inalenga kusambaza silaha zinazotengenezwa nchini kwa maafisa wote wa usalama. Amesema lengo kuu ni kuhakikisha kwamba Kenya inaingia katika biashara ya uuzaji wa silaha katika mataifa jirani.

 

Kwa upande wake Waziri wa Usalama Daktari Fred Matiang'i amesema, serikali imekuwa ikitumia pesa nyingi kununua silaha kutoka nje na hivyo kupata hasara.

 

Serikali hata hivyo itazindua hivi karbuni kiwanda kingine cha kutengeza silaha Mjini Eldoret.

Share this: