×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kamati ya Bunge la Kitaifa wamepiga kupokea hongo

Kamati ya Bunge la Kitaifa wamepiga kupokea hongo

Wanachama wa Kamati ya Utekelezaji katika Bunge la Kitaifa wamepinga madai ya kupokea hongo ili kutatiza uchunguzi kuhusu madai ya uchafuzi wa mazingira dhidi ya Kampuni ya London  Distillers.

Kampuni hiyo imedai kuwa wanachama wa kamati hiyo wamepokea hongo na sasa wanashinikiza kufungwa kwa kampuni hiyo inayotengeneza mvinyo.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Kampuni ya Ederman ikiishtumu kampuni ya London Distillers inayotengeneza pombe dhidi ya uchafuzi wa mazingira kwenye Mto Athi.

Ederman inasema kwamba hali hiyo imeathiri Mto Athi na maeneo jirani huku wakazi wakaathiriwa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Moitalel Ole Kenta amepuuza madai hayo akisema wabunge wamefanya kipaumbele malalamiko ya wakazi wanaothiriwa na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na Landon Distillers.

Naye naibu wake Godfrey Osotsi amesema kuwa wamekuwa wakichuguza madai hayo kwa miaka miwili sasa na kwamba wanasubiri tu ripoti ya mwisho ya uchunguziu kutoka kwa Mamlaka ya Mazingira Nema kabla ya kufanya maamuzi.

Share this: