×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanaharakatai Edwin Kiama aachiliwa kwa dhamana

Mwanaharakatai Edwin Kiama aachiliwa kwa dhamana

Mwanaharakati Edwin Mutemi Kiama ameachiliwa kwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia tano na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Jane Kamau amekataa ombi la Upande wa Mashtka kutaka Kiama azuiliwe kwa siku kumi na nne zaidi ili kutoa nafasi ya uchunguzi. Hakimu Kamau amesema upande huo wa mashtaka haukuwasilisha ushahdi wa kutosha kuonesha kwamba mshtakiwa anafaa kuendelea kuzuilia akisema wana uwezo wa kuufunga ukurasa wake wa Twitter.

Amemwagiza Mutemi kukutana na afisa wa uchunguzi, Patrick Kibowen kwa siku kumi kuanzia leo katika eneo watakalokubaliana kufuatia janga la korona, huku akimwamuru kutochapisha jumbe zozote katika mitandao ya kijamii katika kipindi hicho, kuhusu mkopo wa IMF au Rais Uhuru Kenyatta.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 20 mwezi huu. Kiama ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu alikamatwa jana kufuatia machapisho yake ya kukashifu hulka ya Kenya kuchukua mikopo mara kwa mara. Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya Rais Uhuru.

Kiama amefikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria za Uhalifu wa Mitandaoni Cyber Crime ACT 2018.

Kifungu cha 22 sehemu ya kwanza ya sheria hizo kinasema yeyote anayechapisha kwa kukusudia habari za uongo, za kupotosha au data ya kubuni ama kupitisha habari zisizo za kweli ili kufanya data fulani kuonekana ya kweli, atatozwa faini isiyozidi shilingi milioni 5 ama kifungo kisichozidi miaka miwili, ama adhabu zote mbili.

Sehemu ya pili ya sheria hiyo inahusu uhuru wa kujieleza ambao pia una vipimo au makatazo yake, kwamba ni kosa kuchapisha habari za uongo, za kupotosha au data ya kubuni ama kupitisha habari zisizo za kweli ili kufanya data fulani kuonekana ya kweli.

Kifungu cha 23 kinasema kuwa anayechapisha habari za uongo kwa kukusudia katika kompyuta au vyombo vya habari na kuzua taharuki, vurugu ama kumharibia mtu sifa atatozwa faini isiyozidi shilingi milioni tano, kifungo kisichozidi miaka 10 jela ama adhabu zote mbili.

Share this: