×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Matiang'i kutoa mwelekeo kuhusu Dadaab na Kakuma

Matiang'i kutoa mwelekeo kuhusu Dadaab na Kakuma

Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Fred Matiang'i leo  Alhamisi  anatarajiwa kutoa msimamo kuhusu kufungwa kwa kambi za Kakuma na Daadab baada kukamilika kwa makataa ya kufungwa kwa kambi hizo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi, UNHCR tayari lilikuwa limeishauri  Kenya kuhakikisha kwamba uamuzi wowote itakaochukua utasaidia katika kupatikana kwa suluhu ya kudumu kwa tatizo la wakimbizi.

Kenya ilitoa makataa ya siku kumi na nne kwa UNHCR kubuni njia za kufanikisha kufungwa kwa kambi hizo, japo maisha yamekuwa yaliendelea kama kawaida huku wakazi wakisema huenda kukawa na athari kuu iwapo kambi hizo zitagungwa.

Kambi hizo zimekuwa zikihusishwa na visa vya ugaidi humu nchini ambapo baadhi ya magaidi wamedaiwa kupangia njama hizo katika kambi.

Share this: