×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanahabari apigwa risasi na majambazi

Mwanahabari apigwa risasi na majambazi

Simanzi imetanda kufuatia mauaji ya mhariri wa picha katika Runinga ya KBC, Betty Mutekhele nyumbani kwake katika eneo la Ololua, Kajiado usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa kwamba alifumaniwa na washukiwa watatu wa ujambazi alipokuwa akirejea nyumbani na kuingia naye ndani ambapo waliaamuru wanawe kulala chini.

 Washukiwa hao wa ujambazi walimwagiza Betty kuwapa fedha kisha kumwelekeza katika chumba kingine cha nyumba alikokuwa mumewe na kuwapokonya simu za rununu na vipakatalishi. Baada ya hapo walimpiga risasi mwanahabari huyo na kutoweka. Uchunguzi unatarajiwa kuanzishwa kufuatia kisa hicho.

Share this: