×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wawaniaji wa kiti cha Jaji Mkuu kuchujwa kuanzia Aprili 12

Wawaniaji wa kiti cha Jaji Mkuu kuchujwa kuanzia Aprili 12

Shughuli ya kuwachuja wawaniaji 10 wa wadhifa wa Jaji Mkuu ulioachwa wazi kufuatia kustaafu kwa David Maraga itang'oa nanga Aprili 12 na kukamilika Aprili 23.

Walioidhinishwa kuchujwa ni majaji  Said Chitembwe, Martha Koome, Marete Njagi, Philip Murgor,  Nduma Nderi, Fred Ngatia, William Ouko, Prof. Wekesa Moni, Alice Yano na Prof. Patricia Mbote.  

Kila jaji atatengewa siku nzima ya kufanyiwa mchujo. Wa kwanza kuchujwa atakuwa Jaji Chitembwe tarehe 12 Aprili, yaani Jumatatu wiki ijayo kuanzia saa tatu asubuhi.

JSC aidha imetangaza tarehe 26 hadi 30 Aprili kuwa ya kuwachuja wanaowania wadhifa wa jaji katika Mahakama ya Juu. Wadhifa huo uliachwa wazi kufuatia kustaafu kwa Jaji Jackton Boma Ojwang. 

Share this: