×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Matiang'i aomboleza kifo cha mlinzi wake na mkewe

Matiang'i aomboleza kifo cha mlinzi wake na mkewe

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i ameeleza kusikitishwa na kifo cha Afisa wa Kitengo cha GSU anayehudumu katika wizara yake ambaye amemuua mkewe kwa kumpiga risasi kabla ya kujiua.

Kupitia ukurasa wa twitter, Matiang'i amewataja wawili hao kuwa vijana waliokuwa na maono huku akisema vifo vyao ni ishara ya changamoto za kisaikolojia zinazowakumba baadhi ya maafisa. Matiang'i amesema changamoto hizo zinastahili kushughulikiwa ili kuepusha vifo zaidi.   

Katika kisa hicho cha jana jioni, afisa huyo kwa jina Hudson Wakise ambaye ni mmoja wa walinzi wa Waziri Matiang'i alimuua Pauline Wakasa ambaye pia ni afisa wa polisi katika kitengo cha trafiki, Kituo cha Kilimani jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai, kisa hicho kilitokea katika makazi yao karibu na makao makuu ya GSU, eneo la Ruaraka.

Inaarifiwa kwamba wawili hao walikuwa wakiishi pamoja kabla ya Wakasa kuhamia eneo jingine siku ya Jumamosi karibu na kambi.

Share this: