×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 1,53 waambukizwa korona, 616 wakipona na 18 wakifariki dunia

Watu 1,53 waambukizwa korona, 616 wakipona na 18 wakifariki dunia

Watu wengine 1,523 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona kutokana na sampuli 7, 423 zilizopimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Miongoni mwao 1,432 ni Wakenya huku 91 wakiwa raia wa mataifa ya kigeni.

Aidha,  mtu mchanga ana umri wa miezi mitatu na mkongwe miaka 105.

Kiwango cha maambukizi leo kimepanda na kuwa asilimia 20.5 kulinganishwa na asilima 13.5 ya jana.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuongoza kwa maambukizi mapya ambapo leo watu 626 wameambukizwa ikifuatwa na Kiambu 142.

Watu wengine 616 wamepona korona, 522 walikuwa wakihudumiwa nyumbani na 94 kwenye hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, watu wengine 18 wamefariki dunia kufuatia Covi-19 na sasa kufikisha idadi jumla kuwa watu 2,276

Share this: