
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya ABC Kiseveni kwenye Kaunti ya Machakos ameachiliwa kwa bondi ya polisi baada ya kukamatwa hapo jana akihusishwa na tuhuma za kulenga kufanikisha udanganyifu katika Mtihani wa KCSE.
Naibu Afisa wa Upelelezi wa Machakos Rhoda Kanyi amesema mshukiwa Betta Mutuku Kanyi ameachiliwa huku polisi wakisubiri uchunguzi unaofanyia simu yake kabla ya kushtakiwa.
Kanyi alikamatwa na maafisa wa DCI baada ya karatasi ya pili ya Hisabati kupatikana imechapishwa katika status yake ya Whatsapp.Anadaiwa kuchapisha katarasi hiyo Jumatatu usiku ili kuwawezesha watahiniwa kuyaona maswali katika karatasi hiyo ya jana.
Haya yanajiri huku watahiniwa kumi na watatu waliokamatwa katika Kaunti ya Nyamira wakitarajiwa kushtakiwa leo kufuata udanganyifu katika somo la Kemia.
Awali jana walistahili kushtakiwa kabla ya vikao vya kesi yao kuahirishwa sawa na wenzao wanne wa Kaunti ya Busia
Share this: