
Mwanaharakati wa haki za binadamu Mutemi wa Kiama amefikishwa katika Mahakama ya Milimani kufuatia machapisho yake kuhusu mikopo kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Fedha.
Kiama anahusishwa na chapisho iliyokuwa na picha ya Rais Uhuru Kenyatta na chapisho kwamba shirika la IMF lisimhusishe na Kenya wala kumpa mkopo wowote kwa niaba ya Wakenya. Pia alichapisha nyingine ikiwa na picha ya Naibu wa Rais William Ruto.
Chapisho hilo lilikuwa miongoni mwa machapisho mengine na kauli za Wakenya katika mitandao yao ya kijamii wakilalamikia mkopo wa hivi punde zaidi wa shilingi bilioni 255.7.
Wakenya hao vilevile walisaini rufaa a kulalamikia mkopo huo. Katika kanda iliyonakiliwa akiwa mahakamani, Kiama ameoneka kutojutia machapisho yake na kuendeleza harakati za kuwataka Wakenya kuendelea kuisuta serikali kufuatia maamuzi yake kuhusu masuala mbalimbali.
Share this: