×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya Kilifi imefikia 15

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya Kilifi imefikia 15

Idadi ya watu walioaga dunia kufuatia ajali iliyohusisha mabasi mawili kwenye eneo la Kilifi imefikia watu 15. Kamishna wa Kaunti ya Kilifi, Kutswa Olaka anasema miongoni mwa walioaga dunia ni wafanyakazi wa Kaunti ya Kilifi. Aidha, madereva wa mabasi hayo waliaga dunia papo hapo.

Olaka aidha anasema takribani majeruhi 14 wanatibiwa katika hospitali mbalimbali ikiwamo ya Malindi. Ajali hiyo imetokea kwenye eneo la Kwamkikunyu, Kilifi katika Barabara Kuu ya Malindi – Mombasa ambapo mabasi mawili ya abiria ya kampuni za Sabaki na Muhsin yaligongana ana kwa ana.

Aliyeshuhudia ajali hiyo anasema basi la Kampuni ya Muhsin kutoka Mombasa kuelekea Garissa lilikuwa likipita gari jingine kabla ya kupoteza mwelekeo na kugongana ana kwa ana na basi dogo la Kampuni ya Sabaki lililokuwa likitoka Marerani kuelekea Mombasa.

Share this: