×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

LSK yapinga marufuku ya uagizaji wa chanjo ya Sputnik V

LSK yapinga marufuku ya uagizaji wa chanjo ya Sputnik V

Chama cha Kisheria LSK sasa kinapinga uamuzi wa serikali kupiga marufuku uagizaji wa chanjo dhidi ya virusi vya korona kutoka mataifa ya kigeni na wafanyakazi wa binafsi.

Kupitia ombi mahakamani LSK imesema kuwa marufuku hayo yaliotolewa na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ni kinyume na sheria. Aidha, imesema kuwa hatua hiyo huenda ikisambaratisha juhudi za serikali kukabili maambukizi nchini kutokana na hali kwamba serikali kufikia sasa imeagiza asilimia 30 pekee ya chanjo ambayo haiwezi kuwafaidi Wakenya wote.

Rais wa LSK Nelson Havi, amesema chama hicho kinaitaka serikali kubatilisha uamuzi wa Kagwe na kuwaruhusu wafanyabiashara wa sekta binafsi kuagiza chanjo mbalimbali kwa manufaa ya serikali.

Havi pia anasema wanalenga kuona kuwa mahakama inaingilia katika hatua ya serikali kufutilia mbali leseni za wafanyabiashara hao. Ikumbukwe Kagwe alitoa tangazo hilo baada ya mkanganyiko kuibuka kuhusu chanjo ipi ni bora kati ya AstraZeneca na Sputnik V ya Urusi ambayo inadaiwa kuagizwa kwa wingi na wafanyabiashara.

Haya yakijiri LSK pia inataka serikali kuondoa sitisho la shughuli kwenye Kaunti za Nairobi, Nakuru,Kajiado, Kiambu na Machakos kwa misingi kwamba raia wanakandamizwa huku serikali ikishindwa kuweka mikakati ya kuwakwamua kiuchumi Wakenya.

Havi amesema tangazo la Machi tarehe 26 lililotolewa na Rais Uhuru Kenyattni ukiukaji mkubwa wa haki za Wakenya hasa wakati huu mgumu wa maambukizi.

Share this: