×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Abdul Mohammed Haji atangazwa Seneta wa Garissa

Abdul Mohammed Haji atangazwa Seneta wa Garissa

Sasa ni rasmi kuwa Abdul Mohammed Haji ndiye Seneta wa Garissa.

Tume ya Uchaguzi IEBC imemtangaza Abdul kuwa Seneta wa Kaunti hiyo kupitia tangazo lililochapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali.

Kwenye tangazo hilo, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema kufikian jana hakukuwa na mgombea mwengine ambaye alijitokeza kushindana na Abdul katika uchaguzi huo mdogo ambao ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe kumi na nane mwezi Mei.

Abdulyusuf ambaye ni mwana wa aliyekuwa seneta wa Garissa Yusuf Haji anachukua nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi kufuatia kifo cha babaye.

Jinsi ilivyokuwa kwa babaye, Haji alikuwa aliwania kiti hicho kupitia tiketi ya chama cha Jubilee.

Share this: