×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Muungano wa Madereva wa Masafa Marefu nchini Kenya umeilaumu serikali kwa madai ya kushindwa kuwalinda madereva kutoka Kenya ambao maisha yao yamo hatarani nchini Sudan Kusini.

Mwenyekiti wa Muungano huo, Nicholas Mbugua anasema licha ya serikali kuangazia suala hilo, bado haijaweka mikakati ya kutoa ulinzi kwa madereva wa matrela ambao wamekuwa wakivamiwa kisha kuuliwa na hata magari yao kuteketezwa.

Mbugua amesema zaidi ya madereva ishirini wameuliwa kwa kupigwa risasi na waasi ambao wanapinga serikali ya Sudan Kusini, licha ya serikali kusema ni madereva wawili pekee waliouliwa.

Wakati uo huo, Mbugua amewahimiza madereva kujiepusha na watu wanaojidai kuwa na mpango wa kuwapa ulinzi kupitia nambari inayodaiwa kutumika kukusanya fedha miongoni mwao.

Amesema walaghai wametumia suala la usalama wa madereva wanaosafirisha mizigo kuelekea Sudan Kusini ili kujinufaisha.

Taarifa hii inajiri wakati ambapo baadhi ya madereva wamesitisha shughuli za kusafirisha mizigo kuelekea Sudan Kusini kufuatia utovu wa usalama hasa katika Barabara Kuu ya Yei-Juba.

Ijumaa iliyopita Wizara ya Masuala ya Nchi za Kigeni iliwashauri madereva hao kuwa waangalifu na kwamba mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina ya Kenya na Sudan Kusini ili kuwakabili wahalifu wanaohusika katika uvamizi.

Share this: