×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Vyombo vya habari vilivyofungwa nchini Tanzania vyafunguliwa na Rais Samia

Vyombo vya habari vilivyofungwa nchini Tanzania vyafunguliwa na Rais Samia

Hatimaye vyombo vya habari vilivyofungwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli vimepata afueni baada ya Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan kutangaza kufunguliwa tena.

Akizungumza katika Ikulu jijini Dar Es Salaam, Rais Suluhu aidha ameamuru majarida na magazeti yaliyofutiliwa mbali kuanza kuchapisha japo kwa uangalifu.

Pia ameamrisha kurejeshwa kazini kwa wanahabari waliokuwa wamefutwa kufuatia amri ya Magufuli.
Hata hivyo, Suluhu ameonya kwamba wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria iwapo hawatazingatia sheria za uanahabari.

Pia Suluhu ametangaza kubuniwa kwa kamati ya wataalamu kutathmini hali ya korona katika taifa hilo .        
Amedokeza kwamba kamati hiyo itatoa ripoti kuhusu jinsi ugonjwa unavyosambaa vilevile idadi kamili ya raia ambao wameathiriwa.

Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwaapisha baadhi ya maafisa walioteuliwa kuhudumu serikalini.
Ikumbukwe Tanzania chini ya uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli ilikataa kwamba korona ipo katika taifa hilo na kusitisha utoaji takwimu za kila siku.

Mara ya mwisho mwezi Mei mwaka jana, Magufuli alitoa idadi ya watu waliokuwa wameambukizwa korona ambao walikuwa mia tano, huku vifo vikiwa ishirini pekee.

Kuanzia mwezi Juni mwaka huu, alitoa tahadhari dhidi ya yeyote kutoa matangazo kuhusu ugonjwa wa Covid-19.                   

Share this: