×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Kagwe awalaumu Wakenya kwa ongezeko la maambukizi ya korona

Waziri Kagwe awalaumu Wakenya kwa ongezeko la maambukizi ya korona

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema mapuuza ya Wakenya ndiyo ambayo yamechangia pakubwa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya korona.

Akizungumza wakati wa hafka ya kumkabidhi rasmi Askofu Robert Waihenya wadhifa wa Katibu Mkuu wa Kanisa la PCEA, Kagwe amesema Wakenya hawajali kuhusu masharti yaliyowekwa na serikali ya kudhibiti maambukizi zaidi.

Amesema hulka za Wakenya haziwezi kudhibitiwa na maafisa wakuu serikalini huku akitoa wito kwa kanisa kuingilia kati. Amesema Kanisa li katika nafasi nzuri katika kutoa ushauri na mwongozo katika jamii.

Akizungimzia idadi ya watu wanaofariki kutokana na Covid-19, Kagwe amesema idadi ya vifo nchini ni ya juu zaidi ambavyo ni asilimia 2.7 kulinganishwa na duniani ambavyo ni asilimia 2.2.

Kagwe alikuwa akimwakilisha Rais Uhuru Kenyatta ambaye katika taarifa yake ameahidi kwamba serikali yake itaendelea kushirikiana na kanisa kufanikisha ajenda kwa Wananchi.

Ikumbukwe Waihenya anachukua wadhfa huo kutoka kwa Marehemu Peter Kania, aliyefariki dunia Julai mwaka jana baada ya kuugua Covid-19.

Share this: