×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Matokeo ya KCPE kutolewa wiki mbili zijazo.

Matokeo ya KCPE kutolewa wiki mbili zijazo.

Matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane, KCPE yatatolewa wiki mbili zijazo. Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha ametangaza kwamba usahihishaji wa mtihani unaelekea kukamilika.

Akizungumza katika Kaunti ya Kisumu wakati wa kuongoza shughuli ya kuyafungua makasha ya kuhifadhi mitihani wa KCSE, Mogoha amesema mitihani inayoendelea kusahihishwa sasa hivi ni insha za Kiswahili na Kiingereza lakini usahihishaji wa maswali ya viteuzi ulimalizika.

Waziri aidha amesema masharti ya kudhibiti maambukizi ya korona yanazingatia katika vituo vya kusahihisha mitihani huku idadi ya wanaohusika katika shughuli hiyo ikipunguzwa.

Kuhusu visa vya udanganyifu ambavyo vimeshuhudiwa katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne, KCSE, Magoha amesema kufikia sasa watahiniwa 15 wamekamatwa kwenye maeneo mbalimbali nchini na simu za rununu 15. Magoha hata hivyo amesema watahiniwa hao wataruhusiwa kukamilisha mitihani yao huku uchunguzi ukiendelea.

Share this: