×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mhudumu wa bodaboda ajiua Migori baada ya kumfumania mkewe na mwanamume mwingine katika klabu

Mhudumu wa bodaboda ajiua Migori baada ya kumfumania mkewe na mwanamume mwingine katika klabu

Mhudumu wa bodaboda katika eneo la Uriri, Migori amejiua baada ya kumfania mkewe na mwanamume mwingine katika klabu. Mwili wa jamaa huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyetambuliwa kwa jina, Godfrey Karani ulipatikana jana ukining'inia kutoka kwa paa la nyumba anayoishi.

Kwa mujibu wa Kamada wa Polisi wa Uriri, Peter Njoroge, majirani waligundua jamaa huyo amejiua baada ya kuchukua kipindi kirefu kabla ya kumwona hali iliyowalazimu kuvunja mlango na kuingia chumbani.

Majirani wamewaeleza polisi kwamba alifahamishwa na marafiki kwamba mkewe alikuwa akisakata densi na mwanamume mwingine katika klabu na alipoenda alishuhudia mwenyewe kwamba ni kweli mkewe alikuwa na mwanamume mwingine.

Uchunguzi unaendelea.

Share this: