×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Serikali yashauriwa kuweka mikakati ya kuwasaidia Wakenya wakati huu wa korona

Serikali yashauriwa kuweka mikakati ya kuwasaidia Wakenya wakati huu wa korona

Viongozi wa Kidini kwenye Kaunti ya Meru wamemshauri Rais Uhuru Kenyatta kuweka mikakati ya kuwasaidia Wakenya kiuchumi wakati huu ambapo masharti ya ziada ya kukabili wimbi la tatu la maambukizi ya Korona yanaendelea kutekelezwa.

Katika kikao na wanahabari kwenye Eneo Bunge la Igembe ya Kati, Askofu Mkuu wa Kanisa la  NICA Dayosisi ya Meru, Isiolo na Marsabit - Stephen Kalunyu amesema Wakenya wengi wanapitia hali ngumu kufuatia masharti hayo huku wengine wakipoteza kazi.

Kalunyu ameeleza haja ya serikali kuondoa kodi kwa baadhi ya bidhaa na mishara vilevile kuurejelea mpango wa kuwapa fedha za kujikimu kwa wazee na familia zisizojiweza.

Aidha Kasisi Jacob Kubai wa Kanisa lilo hilo lililoko Meru Kaskazini ameiomba serikali kuweka mikakati ya kuwasaidia wakazi wa Igembe ambao kwa asilimia kubwa wanategemea kilimo cha miraa kujikimu kimaisha. Ameishauri serikali kuitafutia bidhaa hiyo soko la kimataifa, hasa Uropa na Asia.

Wakati uo huo viongozi hao wameiomba serikali kuzidisha kasi ya utoaji wa chanjo dhidi ya korona sawa na magonjwa mengine, mfano polio. Wameisihi kuisambaza chanjo hiyo hadi mashinani.

Share this: