×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wagonjwa wengine 20 wa Covid-19 waaga dunia

Wagonjwa wengine 20 wa Covid-19 waaga dunia

Wagonjwa wengine ishirini wa Covid-19 wameaga dunia katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita na kufikisha elfu mbili mia mbili arubaini na vinne idadi ya vifo vilivyotokana na ungonjwa huo.

Aidha wagonjwa wawili zaidi wa Covid-19 wamelazwa ICU na kufikisha mia mbili kulinganishwa na jana ambapo walikuwa mia moja tisini na wanane huku kumi na saba miongoni mwao wakihitaji uangalizi wa karibu.

Katika takwimu za leo, jumla ya wagonjwa elfu moja mia tano tisini wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali, elfu tano mia tisa tisini na wanane wakihudumiwa nyumbani.

Katika taarifa, Wizara ya Afya aidha imethibitisha kuambukizwa kwa watu wengine mia nne sitini baada ya kupimwa kwa sampuli elfu mbili, mia saba hamsini na tatu. Watu mia nne arubaini na sita ni Wakenya huku kumi na wanne wakiwa raia wa kigeni. Kufikia sasa jumla ya watu elfu mia moja thelathini na tisa, mia nne arybaini na wanane wameambukizwa korona.

Kiwango cha maambukizi leo hii ni asilimia 16.7 kulinganishwa na jana ambapo ilikuwa 15.1. Kaunti ya Nairobi inaendelea kuoongoza kwa watu mia mbili tisini na watano kisha Kitui kwa watu 62 miongoni mwa kaunti nyingine.

Hata hivyo watu wengine mia moja sabini na wanane wamepona Covid-19 , ambapo tisini na tisa walikuwa wakihudumiwa kwenye hospitali mbalimbali na sabini na tisa wakihudumiwa nyumbani. Kwa jumla waliopona Covid-19 kufikia saa ni elfu tisini na nne, mia tatu sitini na mmoja.

Share this: