×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 18 waaga dunia kufuatia Covid-19

Watu 18 waaga dunia kufuatia Covid-19

Watu wengine kumi na wanane wamefariki dunia kufuatia makali ya Covid-19 katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii sasa inafikisha jumla ya walioaga dunia kutokana na ugonjwa huo hatari kuwa elfu mbili, mia mbili ishirini na wanne.

Wizara ya Afya aidha imethibitisha kuambukizwa kwa watu wengine mia tisa kumi na mmoja baada ya kupimwa kwa sampuli elfu sita, arubaini na tano. Katika maambukizi hayo, watu mia nane themanini ni Wakenya huku thelathini na mmoja wakiwa raia wa kigeni. Kwa jumla walioambukizwa korona nchini ni elfu mia moja thelathini, mia tisa themanini na wanane.

Kiwango cha maambukizi leo hii ni asilimia 15.1.  Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi hayo ambapo leo hii watu mia tano thelathini na sita wameambukizwa ikifuatwa na Kiambu kwa watu wengine tisini na mmoja miongoni mwa kaunti nyingine.

Katika takwimu hizo, jumla ya wagonjwa wa Covid-19 elfu moja, mia tano themanini na sita wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali. Aidha wagonjwa elfu tano, mia tisa na watatu wanahudumiwa nyumbani, mia moja tisini na wanane wakiwa wamelazwa ICU, ambapo kumi na wanne wanahitaji uangalizi wa karibu.

Aidha taarifa njema ni kwamba wagonjwa mia tano thelathini na watatu wamepona Covid-19, ambapo mia nne ishirini walikuwa wakihudumiwa nyumbani, na mia moja kumi na watatu walikuwa wakihudumiwa hospitalini. Kwa jumla waliopona ni elfu tisini na nne, mia moja themanini na watatu.

Haya yanajiri huku serikali ikifanikiwa kuwapa chanjo dhidi ya korona watu elfu mia mbili themanini na mbili, mia tano kumi na wanane kufikia jana.

Share this: