×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KEMNAC yasisitiza utaratibu kufuatwa katika kumtafuta Chief Kadhi

KEMNAC yasisitiza utaratibu kufuatwa katika kumtafuta Chief Kadhi

Baraza la Kitaifa la Ushauri wa Dini ya Kiislamu KEMNAC limeishauri Tume ya Huduma za Mahakama JSC kuhakikisha kwamba utaratibu unafuatwa katika kumtafuta atakayejaza nafasi ya Chief Kadhi.

Hatua hii inajiri wakati ambapo Chief Kadhi wa sasa Al Muhdhar Hussein anatarajiwa kustaafu rasmi mwezi Novemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Sheikh Juma Ngao ameshinikiza wadhifa huo utangazwe kuwa wazi baada ya kustaafu kwa Muhdhar ili kutoa fursa kwa wasomi wa dini hiyo kuwasilisha maombi ya kutaka kumrithi Muhdhari kwa mujibu wa sharia.

Aidha ameonya kwamba huenda wakalazimika kuwasilisha kesi mahakamani kupinga kuteuliwa moja kwa moja kwa mrithi wa Muhdhari, likisema kwamba wapo viongozi wengine ambao wamehitimu katika masomo ya dini ambao wanaweza kujaza nafasi hiyo.

Wakati uo huo baraza hilo limeiomba serikali kuongeza kuanza kutekeleza amri ya kutokuwa nje kuanzia saa tano usiku wakati huu ambapo waumini wa dini ya kiislamu wanajiandaa kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani.

Share this: