×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 20 wameaga dunia kutokana na korona

Watu 20 wameaga dunia kutokana na korona

Watu ishirini wamethibitishwa leo kufariki dunia kutokana na makali ya Ugonjwa wa COVID-19, ambapo wawili miongoni mwao wamefariki katika saa ishirini na nne zilizopita.

Wizara ya afya imesema kumi na wanne walirekodiwa kufariki dunia katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, na wanne wamethibitishwa kwamba walifariki dunia kufuatia tathimini iliyofanyiwa rekodi katika vituo mbalimbali vya kiafya.

Idadi hii sasa imefikisha jumla ya watu waliofariki dunia nchini kutokana na korona kuwa elfu mbili, mia mbili na sita.

Aidha, Katika saa ishirini na nne zilizopita,  watu elfu moja,  mia moja themanini na wanne wameambukizwa Korona, baada ya kupima sampuli elfu saba, mia moja thelathini na tisa.

Idadi jumla ya watu walioambukizwa Korona nchini humu sasa ni elfu mia moja thelathini na nane, na sabini na saba.

Viwango vya maambukizi nchini leo hii ni asilimia 16. 5.

Wagonjwa wengine mia mbili ishirini wamethibitishwa kupona COVID-19, hivyo kufanya jumla ya waliopona kufikia leo kuwa elfu tisini na tatu, mia sita na hamsini.

Jumla ya wagonjwa elfu moja, mia tano themanini na wawili wa COVID-19, wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku elfu tano, mia tatu sabini na sita wakiendelea kuhudumiwa nyumbani.

Idadi ya wagonjwa waliolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi inazidi kuongezeka huku leo wakiwa mia moja themanini na saba.

Share this: