×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kampuni zinazonunua na kutoa chanjo dhidi ya korona sharti zifuate sheria

Kampuni zinazonunua na kutoa chanjo dhidi ya korona sharti zifuate sheria

Muungano wa Wanafamasia Nchini PSK umesema unaunga mkono hatua ya serikali kupiga kampuni za binafsi kuagiza chanjo dhidi ya korona kisha kuiuza nchini  bila kufuata sheria.

Rais wa Muungano huo Louis Machogu amesema kwamba iwapo kampuni hizo zitataka kuugiza chanjo kuja humu nchini basi sharti zifuate utaratibu ulioko, kama vile majina na wakurugenzi wa kampuni zenyewe.

Aidha Machogu amesema Wizara ya Afya inastahili kuhakikisha kwamba kampuni hizo zinatumia mfumo wa chanjo System akisema njia hiyo ndiyo itakayorahisisha kufuatilia viwnago vya chanjo na wanaoipokea.

Machogu amesema iwapo kutakuwapo na uwazi basi, Wakenya watafahamu iwapo chanjo wanayopewa ni halali na iwapo imeafikia viwnago vinavyohitajika, ili kujiepushia madhara.

Hapo jana Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alifutilia mbali leseni za kampuni zote za binafsi zilizokuwa zimepata idhini ya kuagiza chanjo kutoka mataifa ya nje.

Waziri Kagwe alisema hatua hiyo ilifuatia mkanganyiko uliokuwa ukishuhudiwa kuhusu chanjo ya Sputink-V iliyokuwa tayari imeanza kutolewa nchini

Wakati uo huo, amesema muungano huo umekuwa ukihudumu bila bodi kwa miaka miwili sasa hali inayolemaza kazi zao, akimwomba waziri Kagwe kubuni bodi hiyo, ili kurahisisha shughuli za kufuatilia masuala muhimu kama yale ya utoaji chanjo.

Share this: