×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwili wa Koinange umezikwa

Mwili wa Koinange umezikwa

Mwili wa Mbunge wa Kiambaa, Paul Koinange umezikwa nyumbani kwake kwenye eneo la Kiambaa, Kaunti ya Kiambu.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo ambayo yamefanywa kwa kuzingatia masharti mapya ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.

Wakati wa hotuba, Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi amesema Marehemu Koinange atakumbukwa kuwa kiongozi mwenye msimamo thabiti katika masuala mbalimbali bungeni.

Amemkumbuka kufuatia juhudi zake za kuwa mwanzilishi wa Maombi ya Kitaifa.

Spika Muturi amekariri kwamba Rais Uhuru Kenyatta aliamini uongozi wa Koinange hivyo kumkabidhi jukumu la kuongoza kamati ya usalama wa kitaifa.

Kando na Kamati ya Usalama katika Bunge la Kitaifa, Marehemu  Koinange pia alikuwa mwanachama wa Kamati ya Afya na ile ya Utungaji sheria.

Ana shahada ya uzamili katika Sheria za Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha International Studies, Athens, Ohio, Marekani, vilevile shahada ya Masuala ya Sosholojia, Anthropolojia na Sayansi ya Siasa kutoka Chuo cha Tarkio nchini Marekani.

Ameaga dunia akiwa na umri wa miaka sitini na tisa

Share this: