×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Uholanzi imesitisha matumizi ya AstraZeneca kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 60

Uholanzi imesitisha matumizi ya AstraZeneca kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 60

Uholanzi ni taifa la hivi punde kusitisha chanjo ya AstraZeneca kwa raia wake walio chini ya miaka sitini.

Maafisa wa afya nchini humo wamesema kwamba hatua hii inafuatia visa vya mgando wa damu miongoni mwa waliochanjwa.

Mafaisa hao wamesema visa vitano vya wanawaka wenye kati ya umri wa miaka 25 na 65 kuwa na mgando wa damu mwilini baada ya kupewa chanjo hiyo vimeripotiwa.

Hatua hii inajiri siku moja baada ya Uingereza kuripoti visa thelathini vya mganda wa damu miongoni mwa watu milioni 18.1 waliochanjwa. Saba miongoni mwa thelathini hao walifariki dunia.

Mapema wiki hii taifa la Ujerumani lilisitisha chanjo hiyo pia kwa raia wake wa chini ya miaka 60.

Mataifa hayoa yamechukua hatua hiyo licha ya Mamlaka ya Kudhibiti Dawa Barani Uropa EMA kutoa hakikisho kwamba AstraZenneca ni salama, baada ya zaidi ya mataifa saba barani humo kusitisha matumizi yake.

Hata hivyo, baadhi ya mataifa likiwamo Italia, Ufaransa na Uhspani yalirejelea matumizi kufuatia hakikisho hilo

Aidha mataifa hayo yanasubiri hadiAprili 7, wakati ripoti nyingine itakapotolewa na EMA kuhusu chanjo hiyo.

Share this: